Kuna mambo kadhaa yanayopaswa kuzingatiwa na mtaalamu wa afya pamoja na wewe katika kuhakikisha shinikizo la damu linalopatikana lina onesha usahihi wa shinikizo la mwili wako. Ili kupata matokeo mazuri kumbuka au mkumbushe dakitari kufuata mambo yafuatayo:
- Kwanza kabisa kabla ya kupima subiri au pumzika kwa muda wa dakika 5 au zaidi kabla ya kipimo kufanyika.
- Hupaswi kuvuta sigara, kunywa kahawa, chai, au kitu chochote kinachoamusha hisia kwa muda wa dakika 30 au zaidi kabla ya kipimo.
- Hakikisha umekaa, miguu ikiwa imefika chini na kamwe isining’inie.
- Hakikisha mikono yako imepumzika kwenye kitu cha kuegemea chenye urefu sawa na msawazo wa moyo wako ulipo.
- Kipimo kinachotumika kupima shinikizo la damu nacho kinapaswa kuwa katika usawa huo wa moyo.
- Hakikisha unapopimwa shinikizo la damu unakuwa hajabanwa na mkojo au haja kubwa
- Hakikisha chumba cha kupimia shinikizo la damu hakina kelele na pia unapopimwa huongei.